UVUVI HARAMU WAZIDI KUHATARISHA MAISHA YA MAMA WAJAWAZITO
TOA MAONI JINA NA MAHALI
Athari ya uvuvi haramu ambazo zimekua zikitajwa kwa watu wanaokula
samaki wanaovuliwa na sumu zimeanza kujitokeza na iwapo hatua ya
kutokomeza ujangiri huu hazitachukuliwa haraka kuna uwezekano wa
watumiaji kupata madhara zaidi ya kiafya.
Baadhi ya athari hizo
ni mimba za wanawake kutoka au kuzaa watoto wenye mapungufu, kupoteza
nguvu za kiume na za kike pamoja na kupata ugonjwa wa kansa.
Samaki ni Kitoweo kilichokua na faida nyingi mwilini mojawapo ni kuwa
na mafuta yenye kiambata aina ya Omega 3 yanayomfanya binadamu kuwa na
uwezo mkubwa wa kufikiri, kutunza kumbukumbu na kuishi kwa muda mrefu.
Uvuvi haramu umebadilisha yote hayo.
January hadi february mwaka huu wanawake 55 mimba zao ziliharibika
lakini hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama ni sumu ya samaki.
Mara nyingi imekua vigumu kwa mlaji kubaini samaki aliyevuliwa kwa sumu
lakini baadhi ya wafanyabiashara wa samaki wanadai kuwatambua.
Feb 30 mwaka huu katika kijiji cha Bukondo majira ya saa 7 usiku wavuvi
haramu 11 wamekamatwa wakiwa na makokoro ya dagaa chini ya mililita 8
ambayo yanauwezo wa kuvua sangara na sato na wengi wao ni vijana
wanaotumiwa kufanya shughuli hizi.
No comments:
Post a Comment