Maelezo Mafupi Kuhusu Vyuo Vya Maendeleo Ya Jamii

1.0. Utangulizi:
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ina vyuo tisa (9) vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Cheti cha Msingi, Cheti, Stashahada na Shahada kama ifuatavyo:-
(i) Chuo cha Tengeru kinatoa Shahada ya kwanza kwa muda wa
miaka mitatu katika Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo na katika
upangaji na uendeshaji Shirikishi wa Miradi.
(ii) Chuo cha Missungwi kinatoa Stashahada ya Maendeleo ya Jamii Ufundi kwa muda wa miaka miwili.
(iii) Vyuo vya Buhare, Rungemba na Monduli vinatoa Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kwa muda wa miaka miwili
(iv) Vyuo vya Ruaha, Uyole na Mlale hutoa mafunzo ya Maendeleo
ya Jamii katika ngazi ya cheti cha Msingi kwa muda wa mwaka mmoja na
Cheti kwa muda wa miaka miwili.
(v) Chuo cha Mabughai Lushoto hutoa mafunzo ya Maendeleo ya
Jamii Ufundi katika ngazi ya cheti cha Msingi kwa muda wa mwaka mmoja na
cheti kwa muda wa miaka miwili.
Madhumuni:
- Kutoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwa wahitimu wa
kidato cha nne na sita waliotoka moja kwa moja mashuleni.
- Kuendeleza maafisa walioko kazini wenyewe taaluma ya Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii;
- Kupata wataalamu mahiri walio na uwezo wa kuiwezesha jamii kujiletea maendeleo yao wenyewe.
- Kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji sanjari na mabadiliko yanayotokana na utandawazi, sayansi na teknolojia.
- Kudurusu mitaala iliyopo ili iweze kukidhi mahitaji ya jamii kwa wakati muafaka
No comments:
Post a Comment